Mbunge mpya mwanamke Lauren Boebert, ambaye ni Mbunge kupitia Chama cha Republican huko Washington DC Marekani ameahidi kutembea na bunduki wakati wote wa muhula wake.

Boebert amesema yeye kama mwanamke mwenye urefu wa futi tano, na uzito wa kilogramu 45, anachagua kujilinda mweyewe kwa sababu yeye ndio mlinzi mzuri kwake binafsi hivyo atajilinda mwenyewe kwa kushika bunduki.

Wakati wa kipindi cha kampeni za Marekani kuelekea uchaguzi Mkuu Boebert alikuwa anasisitiza suala la kumiliki na kutembea na bunduki.

Mkuu wa Polisi wa Washington DC Robert Contee amesema mbunge atakabiliwa na adhabu ileile kama mtu mwingine yeyote anayepatikana akiwa amebeba silaha katika mji wa Washington DC.

Sheria za umiliki wa Bunduki nchini Marekani ziko tofauti kutokana na Majimbo na Wabunge wanaruhusiwa kumiliki bunduki katika ofisi zao na kusafiri nazo mjini Washington DC mradi zisiwe na risasi.

Kauli ya Mbowe kwa Mbunge wa Nkasi Kaskazini
Afisa Mkuu Georgia asema Trump ni muongo