Mbunge wa wa Jimbo la Mbeya mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.(CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Mr.II Sugu’ leo tarehe 31/08, 2019, amefunga ndoa na mpenzi wake Happiness Msonga, katika kanisa Katoliki Ruanda Jijini Mbeya.

Mmoja wa watu maarufu na mwanasiasa ambaye ni mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule maarufu kwa jina la Prof. Jay amewapa pongezi kwa kutuma picha na video katika mitandao ya kijamii ya Instgram na Twitter ambapo ameandika,

“Muda wa Kanisani harusi ya Jongwee, Mbeya stand up , Hongereni sana kaka yangu @jongwe__ na Shemeji yetu Happiness msonga kwa kukamilisha ndoa yenu takatifu leo, Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu Awabariki zaidi na awasimamie kwenye Maisha yenu ya NDOA, AMEN”

Mr II Sugu kabla ya kufunga ndoa na mke wake huyo wa sasa alikuwa na mahusiano na mfanyabiashara na muigizaji Faiza Ally na walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike.

Mbunge mwingine ambaye amempongeza Sugu ni Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye

RC Chalamila alivuruga jiji la Mbeya, 'Hawa wamechokoza nyuki'
RC Makonda awashangaa Chadema, 'Akili ndogo haiwezi kujadili mambo makubwa'