Wakati zoezi la uopoaji miili ya wahanga wa ajali ya maji iliyotokana na kivuko cha Mv Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Kisiwa cha Ukara na Bugorora wilayani Ukerewe, Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi amesema kivuko hicho kilifanyiwa ukarabati.

Amesema kuwa Kivuko hicho kilifanyiwa ukarabati miezi miwili iliyopita, hivyo kilikuwa sawa na kilikuwa mbioni kubadilishiwa ratiba ikiwemo kuongeza idadi ya safari ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa eneo hilo.

“Kuhusu hoja yangu niliyoitoa bungeni, ilifanyiwa kazi ambapo tulikuwa tunahitaji injini mbili ambazo zilipatikana na zikafungwa labda tu suala ambalo lilikuwa bado tunalifanyia kazi ni kuona namna gani tunaweza kubadilisha idadi ya safari”, amesema Mkundi

Aidha, amesema kuwa yeye mwenyewe ni miongoni wa watu waliopoteza ndugu katika ajali hiyo ambapo amedai kuwa takribani ndugu zake watatu wamefariki kwenye ajali hiyo.

 

 

Lukuvi apiga marufuku kampuni binafsi kupima ardhi
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 22, 2018