Vita dhidi ya ugonjwa wa malaria ikiwa inaendelae ulimwenguni, wanasayansi nchini Uingereza na Gambia wamefanikiwa kuwafunza mbwa kutambua harufu ya malaria kwa kutumia nguo za watu mwenye maambukizi.

Wanasayansi hao wametoa taarifa kuwa wana ushahidi wa awali unaoonesha kuwa mbwa wanaweza kunusa malaria japokuwa utafiti huo upo katika hatua za awali wanaamini kuwa matokeo yake yanaweza kubadili namna ya kutumia vipimo vya malaria.

Kwa mujibu wa tafiti za hapo awali, mtu ambaye anavimelea vya malaria mwilini anakuwa na harufu tofauti ambayo inawavutia mbu kuendelea kumshambulia na kwa sababu hiyo mbwa wapo kazini kuinusa harufu hiyo.

Pia mbwa hao wapo kwenye mafunzo ya kunusa saratani na ugonjwa hatari wa kukakamaa (parkinson’s disease)

Mtafiti Mkuu kutoka chuo cha Durham, Profesa Steve Lindsay , amesema wanafuraha kubwa juu ya matokeo waliyoyapata kutoka kwa mbwa hao na wanaendelea kujiridhisha kama wanauwezo wa kutambua aina mabalimbali za malaria lakini mbwa hao bado hawajawa tayari kutumika kila siku.

Profesa Steve alimalizia kwa kusema utumiaji wa wanyama hao pia utakuwa ni hatua kubwa katika kutokomeza ugonjwa wa malaria.

 

Tatizo si kukamata mashoga- RC Mwanri
Video: Kiherehere champonza Zitto, DCI aibua mapya Kibiti