Uongozi wa Dodoma Jiji FC umevunja mkataba na Kocha Mbwana Makata leo Jumatano (Februari 23), baada ya makubaliano ya pande hizo mbili.

Dodoma Jiji FC wamethibitisha kuachana na Kocha huyo ambaye amekua kwenye Benchi lao la Ufundi kwa misimu mitatu, tangu klabu hiyo ilipopanda Daraja msimu wa 2018/19.

Taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo imeeleza kuwa, mwenendo mbaya wa matokeo ya kikosi chao katika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’, imekua sababu ya pande hizo kuachana kwa amani.

Hata hivyo Uongozi wa Dodoma Jiji FC umemshukuru Kocha Mbwana Makata kwa kazi kubwa aliyoifanya klabu hapo kwa kipindi chote, na umemtakia kila la kheri katika maisha yake mapya.

Dodoma Jiji FC kwa sasa ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku mwishoni mwa juma lililopita iliondoshwa kwenye Michuano ya Kombe la Shiriskiho ‘ASFC’ kwa kufungwa na Pamba FC ya Jijini Mwanza kwenye Hatua ya 16 Bora.

Florent Ibenge: Simba SC haitanionea tena
Balozi Mbarouk amuaga Balozi wa Vatican