Mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta amesema Young Africans kama ikijipanga inaweza kuifunga TP Mazembe katika mechi yao ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Young Africans itacheza na TP Mazembe ya DR Congo kati ya Juni 28 na 29, mwaka huu jijini Dar es Salaam mchezo wa kwanza wa Kundi A la Kombe la Shirikisho.

Samatta aliyewahi kuichezea TP Mazembe akitokea Simba, amesema amesema anaamini hilo linawezekana kwani kikosi cha Young Africans hivi sasa kipo vizuri ukilinganisha na misimu mingine iliyopita.

“Hali hiyo ndiyo inayonifanya niamini kuwa Yanga inaweza kuifunga TP Mazembe, kwani nimekuwa nikiifuatilia sana na kuona jinsi wachezaji wake wanavyopambana uwanjani.

“Hata hivyo Yanga wanatakiwa kujipanga na kukiandaa kikosi chao kwa ajili ya michuano hiyo, kama kuna upungufu ambao waliuona hapo awali basi muda huu ndiyo wa kuufanyia kazi kabla ya kuanza kwa hatua hiyo makundi.

“TP Mazembe ni timu nzuri na yenye mafanikio Afrika, lakini katika soka lolote linaweza kutoka ndiyo maana nimesema Yanga inaweza kuifunga timu hiyo kama ikijiandaa vizuri,” alisema Samatta ambaye leo ataichezea Taifa Stars dhidi ya Misri.

Los Cafeteros Yachanua Mbele Ya Wenyeji Wa Copa America 2016
Ray Leonard, MIke Tyson Watoa Heshima Zao Za Mwisho