Nyota ya nahodha wa Taifa Stars na mchezaji wa klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta inaendelea kuongeza mng’ao na kuzivutia klabu kubwa duniani, na sasa imekuwa zamu ya klabu iliyomuibua mchezaji wa Juventus na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, Sporting Lisbon au Sporting CP.

Klabu hiyo imeripotiwa kufanya mazungumzo na KRC Genk wakiwa na matumaini ya kumsajili Samatta ambaye msimu uliopita alipachika magoli 23 na kuiwezesha klabu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza ya Ubelgiji na kupata nafasi ya kushiriki michuoano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu huu.

Samatta ambaye msimu uliopita alishinda tuzo ya Ebony Shoe, kama mchezaji bora wa Afrika anayecheza Ligi ya Ubelgiji, amewahi kuwaniwa na klabu kama Burnley, Watford, Everton, West Ham na Cardif.

KGR Genk walizitaka Euro Milioni 12 zilizokuwa kisiki kwa timu hizo kumnasa ‘Sammagoal’.

Klabu ya Sporting CP ambayo inasubiri saa kadhaa kuona kama itafanikisha kumnasa Samatta kwakuwa dirisha la usajili barani ulaya linafungwa leo, wana historia ya kumlea Ronaldo hadi mwaka 2003 aliponyakuliwa na klabu ya Manchester United.

Mrithi wa Tundu Lissu kuapishwa kesho bungeni
JPM awapa watendaji wa kata nguvu kuwabana mawaziri, ma-RC 'usiogope kumlima'