Nahodha na mshambuliaji wa  timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Samatta hatakuwepo kwenye kikosi kitakachomenyana na Burundi leo jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Samatta aliyefunga mabao yote katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana Jumamosi, amelazimika kurejea ili kuwahi maandalizi ya klabu yake kwa mchezo wa Robo Fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Celta de Vigo nchini Hispania Aprili 13.

Kwa kumkosa Samatta, kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amemuanzisha Ibrahim Hajib kama mshambuliaji kiongozi akicheza na kiungo Farid Mussa, huku pembeni akiwatumia kiungo Muzamil Yassin kulia na winga Simon Msuva kushoto.

Kwa ujumla kikosi cha Stars leo kipo hivi; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Salim Mbonde, Himid Mao, Muzamil Yassin, Salum Abubakr ‘Sure Boy’, Ibrahim Hajib, Farid Mussa na Simon Msuva.

Katika benchi watakuwapo Said Mohammed, Hassan Kessy, Gareiel Michael, Hassan Kabunda, Jonas Mkude, Mbarak Yussuf, Abdulrahman Juma, Shiza Kichuya na Frank Domayo.

Thierry Henry Kumrithi Arsene Wenger
Young Africans Na Tanzania Prisons Kucheza April 22