Mc Pilipili amejishindia tuzo ya kuwa kijana bora katika nyanja ya uchekeshaji kwa mwaka 2017 (Youth Comedian of the year), tuzo hizo za Scream Awards  zimetolewa nchini Nigeria, na Mc Pilipili kutoka Afrika Mashariki amaiwakilisha vyema Tanzania kwa kuibuka kidedea na tuzo hiyo.

Kwenye kipengele hicho Mc Pilipili ameshindanishwa na wakali wengine wachekeshaji kutoka nchi nyingine wakiwemo Kenny Blaq, Emma Oh My God, Arole & Asiri                Josh2funny kutokea Nigeria, Kalybos kutokea Ghana na wengine wengi.

 

Kisa cha walimu tisa kufukuzwa kazi
Mwanachama wa NCCR- Mageuzi ajivua uanachama