Mchekeshaji  Emmanuel  Mathias  maarufu kama MC Pilipili amesema ana ndoto za kuwa mbunge, huku akiwa anafanya harakati nyingi ikiwemo kuutangaza mji wa Dodoma kupitia sanaa ya uchekeshaji.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Dar24 mwishoni mwa wiki, MC Pilipili amesema kuwa katika ndoto za kuwa mbunge yote yanawezekana  lakini anaamini Mungu akipenda au chama chake  CCM  kikiweza kumteua kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo alisema jamii inapaswa kujua kuwatumia wananchi si lazima uwe umechaguliwa kuwa kiongozi bali hata wewe mwenyewe kuguswa  na kuanza kufanya hivyo ni uongozi pia.

”Ndio maana sasa hivi nimeelekeza nguvu zangu katika mji wa Dodoma, ambapo kuna mambo mengi watu wanapaswa kuyajua, yaliyofanywa huko nitakayoyatangaza kupitia ‘MC Pilipili Comedy Festival’ itakayofanyika huko septemba 28 mwaka huu, ‘’ mchekeshaji huyo ameiambia Dar24.

Amesema  kuwa katika kuhakikisha watu wa mkoa huo wanapata ladha zilizokuwa zikiishia Dar es Salaam pekee, amewapelekea mchekeshaji kutoka nchini Kenya Eric Omond.

Aidha, amesema kuwa katika show hiyo atataja mambo 10 ambayo wengine hawayajui  yameshafanywa katika mji huo wa kitaifa na kuwezesha kutumika kama fursa katika kujiletea maendeleo huku akiwataja baadhi ya wasanii watakao sindikiza shoo hiyo ni pamoja na Dullyvani, dogo pepe, Ally na Oscar nyerere huku bendi ya TNC ikitumbuiza.

Video: Rostam wamponda Billnass kwa Nandy
Diamond aitika wito wa serikali