Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Amos Makalla leo Juni 7, 2021 amefanya kikao cha pamoja na Maafisa Afya na Mazingira kutoka Wilaya tano za Mkoa kwa lengo la kujadiliana hatua za mwisho za ukamilishaji wa mpango mkakati wa kuifanya Dar es salaam kuwa Safi.

Katika kikao hicho RC Makalla alitaka kujua ni mambo gani yamekuwa kikwazo kwao hadi kusababisha Jiji kuwa katika hali ya uchafu na nini kifanyike ili kampeni ya usafi inayopangwa kuanza hivi karibuni iweze kuwa na mafanikio makubwa.

Amesema lengo lake ni kuona Dar es salaam inakuwa katika hali ya usafi kwakuwa Jiji hilo linabeba taswira ya Nchi na ndilo linalopokea wageni wa mataifa mbalimbali hivyo ni lazima liwe kwenye hali ya usafi. 

Mei 28 RC Makalla alifanya kikao na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Makatibu tawala na kuwapatia maagizo nane ya kushughulikia ikiwemo suala la Usafi wa Jiji ambapo ajenda ya usafi ni moja ya vipaumbele muhimu alivyopanga kuanza navyo.

Makala ameagiza kila Halmashauri kuhakikisha kampuni zinazopewa tenda ya usafi ziwe na sifa ikiwemo kuwa na vitendea kazi vya kutosha.

Bodi ya mikopo kufungua dirisha Julai Mosi
Agizo la Waziri kwa TFNS, MUHAS, SUA na TBS