Wakati Mashabiki wengi wa Soka Duniani wakidhani kwamba mchakato wa kuuzwa kwa Klabu ya Manchester United umeshafeli na kuna uwezekano isiuzwe kabisa, taarifa za moto kutoka tovuti ya The Sun ni kwamba mchakato bado upo pale pale na siku chache zijazo matajiri wengine huenda wakatua jijini Manchester kwa ajili ya majadiliano zaidi.

Changamoto kubwa inayotokea kwa sasa ni msuguamo wa familia ya Glazers ambayo ndio mmiliki wa timu hii, baadhi ya wanafamilia wanataka iuzwe kwa kiasi cha pesa ambacho wanunuajia wamefikia kwa sasa na wengine wanagoma, lakini wanaotaka iuzwe ni wengi kuliko wanaogoma.

Hofu ya kwamba Mashetani Wekundu hawauzwi tena ilibuka baada ya kimya cha muda kutoka wamiliki wa timu wakati ambao ofa kutoka kwa matajirimbalimbali zimewasilishwa.

Sheikh Jassim bin Hamad Al-Thani wa Qatar sambamba na Muingereza Sir Jim Ratcliffe wote wanadaiwa kuwasilisha ofa ya Pauni 5 bilioni, ambayo ndio inadaiwa kuwa ni pungufu ya kiwango ambacho wamiliki wa timu hiyo wanataka na tangu ofa hiyo iwasilishwe hawajapata mrejesho wowote na siku zina- zidi kukatika.

Lakini vyanzo vya karibu na timu hiyo vimefichua kwamba awali familia ya Glazers ilihitaji kiasi kisichopungua Pauni 6 bilioni na imewaita tena Al-Thani na Sir Jim kwa ajili ya majadiliano zaidi kuona kama watakuwa tayari kupanda dau zaidi.

Lakini baadhi yao wanaona ni vyema kuchukua kiasi hicho cha pesa hata kama vigogo hao watagoma kutoa Pauni 6 bilioni.

Ikiwa kwenye vikao hivyo ya mwisho matajiri hawa hawatofikia bei ambayo Joel na Avram Glazer wanaihitaji, wawili hao wataendelea kuingoza timu hiyo lakini watauza hisa nyingi na kuchukua kiasi hicho cha pesa kuwapa ndugu zao wanaohitaji timu iuzwe kisha wao wataendelea kusalia na hisa chache.

Rwanda yaadhimisha kumbukumbu mauaji ya Kimbari
Kashfa ya mabati: Waziri, kaka yake kula Pasaka Jela