Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti na Utumishi wa Umma, Mohamed Mchengerwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa dosari za fedha katika taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo zilizotajwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Ametoa agizo hilo wakati akijitambulisah kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri ambapo ametaka apewe majibu ya uchunguzi huo kabla ya Aprili 28, 2021.

Amesema ripoti ya CAG ya ukaguzi wa Serikali kuu ya mwaka 2019/20, ilionyesha katika Chuo cha Utumishi wa Umma kuna mapato ambayo hayakupokewa yenye thamani ya Sh. 284.8 milioni na matumizi yasiyolipwa ya Sh 2.301 bilioni.

Aidha, Mchengerwa amesema kuwa Ofisi yake itatekeleza maagizo yote yalitolewa na Rais Samia, ikiwamo TAKUKURU kufanya uchunguzi wa upotevu wa fedha katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Deogratius Ndejembi, amesema ili kujenga maadili kwa watumishi kuna haja ya kukitumia vyema chuo cha utumishi wa umma.

Ndugai aonya wabunge kutumia usafiri wa bodaboda
Balozi Mulamula aanza kazi rasmi

Comments

comments