Johansen Buberwa – Kagera.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema atawachukulia hatua za kisheria Viongozi wa kisiasa na Serikali ambao wapo kwa ajiri ya kukwamisha Miradi ya Maendeleo ambayo inatekelezwa Katika Manispaa ya Bukoba na Mkoa wa Kagera.
Mchengerwa ameyasema hayo wakati akishudia uwekaji Saini Katika Mikataba ya Usanifu wa Miradi ya uboreshaji Miundombinu ya Miji 15 ya Kundi la Pili ambayo itaghalimu zaidi ya Shilingi Trilioni moja, inayofanyika katika Manispaa ya Bukoba.
Amesema, wapo baadhi ya Viongozi ambao wanaokwamisha maendeleo ya Bukoba na Mkoa wa Kagera na kusema kuwa yeye kama Waziri atashughulika nao.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajath Fatma Mwassa ameishukuru kwa kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Stendi ya Kisasa na Soko la Kisasa ambalo limekuwa na changamoto kwa muda mrefu.