Shirikisho la soka nchini Cameroon FECAFOOT, limethibitisha kutokea kwa kifo cha mchezaji wa klabu ya Dynamo de Douala inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humio

Leopold Angong Oben, mwenye umri wa miaka 26, alionekana akianguka katika eneo la hatari la timu pinzani ya Colombe du Dja-et-Lobo katika uwanja wa Reunification uliopo mjini Douala.

Jopo la watoa huduma ya kwanza uwanjani hapo lilijitahidi kufanya shughuli yake ya kumpatia matibabu mchezaji huyo, lakini mambo yalikua magumu kufuatia vipimo vya awali kuonyesha alipata mshutuko wa moyo.

Wachezaji na watu wa waliokua karibu na eneo la kuchezea walionyesha ushirikiano wa kutoka kwa jopo hilo, lakini bado mambo yalikua magumu, na ndipo ilipoamriwa apelekwe kwenye hospitali ya taifa ya mjini Douala.

Hata hivyo dakika chache mara baada ya kuondolewa uwanjani, Leopold Angong Oben alipoteza maisha.

Tukio la kuanguka kwa mchezaji huyo lilitokea katika dakika ya 33 ya mchezo huo wa ligi daraja la pili.

Oben, anakua mchezaji wa pili wa klabu ya Dynamo de Douala kufanriki dunia baada ya mlinda mlango Ferdinand Mbog aliyekua na umri wa miaka 27, kupoteza maisha majuma matatu yaliyopita kufuatia majeraha yaliyokua yakimkabili.

Juventus Kukamilisha Ya Juan Cuadrado Leo
Bolt Adhihirisha Ubora Wake Mjini Beijing