Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa mchezaji wa timu ya vijana wa chini ya miaka 17 wa Jamhuri ya Congo-Brazzaville, Langa Lesse Bercy, aliyetakiwa kufanyiwa vipimo vya umri leo hakufanya hivyo, kinyume na makubaliano yaliyofikiwa.

Kwa mujibu wa TFF, Jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuwa mchezaji huyo ameshindwa kusafiri kwenda Cairo Nchini Misri kwa kuwa yuko katika eneo lililoko ‘vitani’ lakini eneo hilo halikutajwa.

Awali, CAF liliagiza apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo, lililoko Cairo, Misri kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging Resonance).

TFF kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, imesema kuwa itaendelea kufuatia kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha haki inatendeka.

Zoezi la kufanyika kwa vipimo hivyo lilinza baada ya TFF kudai kuwa haijaridhika na imejiridhisha kuwa mchezaji huyo alikiuka kanuni za mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Hivyo, ikaamua kukata rufaa CAF.

Madiwani watakiwa kupima ardhi haraka, kujiandaa na uwekezaji
Majaliwa ampa siku 18 Mkandarasi kukamilisha umeme Mlandizi