Imefahamika kuwa kuna mchezaji mpya wa Young Africans huenda akatambulishwa kupitia mkutano mkuu wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika keshokutwa Jumamosi (Juni 24) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.

Katika mkutano mkuu wa mwisho kufanyika mwaka jana ambao ulikuwa na ajenda pia ya uchaguzi mkuu ambapo alipatakana mshindi ambaye ni Rais wa sasa Injinia Hersi Said, Wanachama wa Young Africans walipewa sapraizi.

Hersi baada ya kutangazwa kuwa Rais wa Young Africans, alimtambulisha aliyekuwa kiungo wa Newcastle United ya England, Gael Bigirimana na kuibua shangwe zito japo usajili huo haukulipa.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Young Africans kinaeleza kuwa uongozi wa Young Africans huenda ukawapa sapraizi nyingine ya usajili wa mchezaji huku pia kukiwa na taarifa za kumshusha mmoja ya wachezaji ambaye tayari kila kitu wamemaliza na kumtambulisha siku hiyo ya uchaguzi mkuu.

“Young Africans kwenye mkutano huu mkuu huenda wakamshusha mchezaji wa maana na kumtambulisha kama ambavyo walifanya kwa Gael Bigirimana msimu uliopita ambapo walimtambulisha kupitia mkutano mkuu.

“Kama ambavyo unafahamu kuwa kwa sasa ndani ya Young Africans kuna mambo mengi yanaendelea haswa kwa wachezaji wanaoachwa na wale walioondoka kama Kocha Mkuu Nasreddine Nabi na kocha wa makipa Milton Nienov.

“Hivyo kwa wale watakaoingia huenda kupitia mkutano mkuu akatambulishwa mchezaji mmoja kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wananchi wanapata amani juu ya usajili wa msimu huu,” kimesema chanzo hicho.

Eden Hazard: Bado ninaweza kupambana
Punda wasababisha maandamano Kenya