Mtanzania Charles Misheto amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu ya Rabestein FC ya nchini Ujerumani.

Rabestein FC inashiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ujerumani na Mishetto aliyekuwa kiungo wa zamani wa Stand United ya Shinyanga, tayari amesaini makataba huo.

Akizungumza kutoka Ujerumani, Mishetto amefanikiwa kusaini mkataba na timu hiyo.

“Ingawa awali nilikuwa nafanya majaribio na timu nyingine, lakini sasa nimefanikiwa kusajiliwa na timu nyingine ya daraja la nne ambayo ilianza kuniwania,” alisema.

“Nilikuja hapa, nikafanya nao mazoezi kwa siku mbili, baada ya hapo wamekubaliana na uwezo wangu, tumesaini mkataba.”

Juventus Yazipiku FC Barcelona, Real Madrid Tuzo Za UEFA
Migi Rukhsa Kuitumia Azam FC Kagame Cup