Kamati ya uendeshaji na Usimamiso wa Ligi ya Bodi ya Ligi kuu Tanzania ‘TPLB’ imemfungia michezo mitatu mchezaji wa Ruvu Shooting Faid Said na kumtoza faini ya Shilingi 500,000 kwa kosa kukwepa kupena mikono na wachezaji wa Tanzania Prisons pamoja na waamuzi.

Faird alifanya kitendo hicho katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya Februari 20.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 41:5 (5.4) ya ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Kamati hiyo pia imetangaza kuipa onyo klabu ya Tanzania Prisons kwa kosa la Shabiki wake mmoja kuingia Uwanjani wakati wa kipindi cha Pili kikielea kuanza. Onyo hilo limetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 17 (18) na 17 (60) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za Mchezo.

Uingereza yazuia dili la Chelsea FC
Mfumo mpya wa kununua umeme kuanza Julai