Beki wa zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya England Kenny Sansom, amelazwa hospitali kufuatia kuzidisha unywaji wa pombe kali uliopindukia.

Awali taarifa zilizeleza kuwa mkongwe huyo amelazwa kwa kuhofiwa ana maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19), lakini taarifa hizo zimekanushwa na klabu ya Arsenal ambayo kwa sasa ipo karibu sana na familia yake.

Mkongwe huyo ambaye alibeba jukumu la kumkaba nahodha wa Argentina Diego Maradona kwa wakati huo, kwenye mchezo wa robo fainali wa fainali za kombe la dunia mwaka 1986, lakini alishindwa kuzuia bao la mkono ‘Hand of God’ lililofungwa na mshambuliaji huyo ambaye alitamba kwa kupasua ngome za ulinzi za timu pinzani.

“Kenny kwa sasa amelazwa hospitali. Anaangiliwa kwa ukaribu na madaktari, amefamnyiwa vipimo, amebainika hana maambukizi COVID-19, tatizo ni unywaji wa pombe uliopindukia” umeeleza ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wa Twitter wa klabu ya Arsenal.

Former England footballer Kenny Sansom opens heart on alcohol ...
Picha ya Kenny Sansom iliyopigwa hivi karibuni.

Ujumbe huo umeongeza kuwa, hali ya mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 61, hairidhishi lakini madaktari wanaendelea kufanya juhudi ili kuyaokoa maisha yake.

Sansom, aliitumikia timu ya taifa ya England katika michezo 86 kati ya mwaka 1979 na 1988, pia amecheza michezo 394 akiwa na klabu ya Arsenal.

Eritrea : wagonjwa wote wa Covid -19 wamepona
Mshindi wa BSS apokea sehemu fedha anazodai