Mchezaji wa zamani Timu za Simba, Pamba, Reli na Timu ya Taifa ya Tanzania, Amri Ibrahimu amefariki ghafla usiku wa kuamkia leo Aprili 9, 2023 nyumbani kwake mtaa wa Sabu Mkoani Morogoro.

Akithibitisha kutokea kwa msiba huo, Mwenyekiti wa mtaa wa Sabu, Beno Mluge amesema siku ya tukio marehemu hakuonekana kutwa nzima ndipo walipoenda chumbani kwake na kukuta mlango ungefungwa na walipofungua wakakuta amefariki akiwa mlangoni.

Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa Morogoro na Mstahiki Meya, Pascal Kihanga amesema marehemu alicheza mpira miaka ya 1980 ambapo licha ya kuleta mafanikio nchini pia amewahi kua kocha wa Timu za Rinho Rangers na Ndanda Fc.

Hadi umauti unamkuta Marehemu Amri alikua anafundisha Timu mbalimbali huku Mbunge wa Morogoro mjini Abdulazizi Abood akichukua jukumu la kumsimamia msiba huo na mazishi ambayo yalifanyika kata ya Lukobe, Mkoani humo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo April 10, 2023
Usiyoyajua kuhusu Siku kuu ya Pasaka Duniani