Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Mabingwa watetezi Yanga SC na Maafande wa JKT Ruvu uliokuwa ufanyike Jumatano ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeahirishwa.

Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ya Shirikisho la soka nchini TFF , imethibitisha kuwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na JKT Ruvu ya Pwani, ulipangwa kufanyika Jumatano Agosti 31, 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam imeahirishwa mpaka itakapopangiwa tarehe nyingine.

Hatua hiyo baada ya Yanga kuomba uahirishwe kwa sababu ina wachezaji wengi katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars.

Wachezaji hao ni Deogratius Munishi ‘Dida’,Vincent Andrew ‘Dante’,Kelvin Yondani na Mwinyi Hajji, kiungo Juma Mahadhi na Simon Msuva.

Wakati huohuo Yanga pia imesema wachezaji wake wengine,Vincent Bossou (Togo), kiungo Haruna Niyonzima (Rwanda) na mshambuliaji Amissi Tambwe (Burundi) nao pia wameitwa na timu zao za taifa na kufanya idadi ya wachezaji kufikia wanane.

Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinaruhusu timu ambayo wachezaji wake wasiopungua watano wameitwa timu za taifa kuahrishiwa mechi.

 

Rais Malinzi Atuma Salamu Za Rambirambi Msiba Wa Munishi
Kipa Aliyeinyima Ulaji Simba SC Aitwa Taifa Stars