Mchoro wa miaka 500 wa Yesu ambao unaaminiwa kuwa ni wa Leonardo da Vinci, unapelekwa katika makazi ya Louvre huko Abu Dhabi.

Katika taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya habari imesema kuwa mchoro huo umenunuliwa na mtoto wa mfalme nchini Saudi Arabia.

Aidha, mchoro huo unaofahamika kama Salvator Mundi au (mkombozi wa dunia) uliuzwa jijini New York kwa dola za Marekani milioni 450. hivyo kuweka historia ya kuuzwa kwa fedha nyingi zaidi katika historia.

Gazeti la The New York Times limeripoti kuwa mchoro huo umenunuliwa na Bader bin Abdullah bin Mohammed bin Farhan al-Saud.

Hata hivyo, Leonardo da Vinci alifariki mwaka 1519 na kuacha michoro zaidi 20 maarufu inayojulikana hadi hivi sasa.

 

 

 

Chanzo cha mwandishi kupotea chatajwa
Vigogo kukutana hatua ya mtoano Ulaya