Mchungaji Thom Miller mwenye umri wa miaka 60 amewashangaza wengi baada ya kuamua kumuoa binti aliyempa ujauzito huku mkewe akiibariki ndoa hiyo.

Mchungaji huyo wa Jimbo la Ohio nchini Marekani aliiambia Bacrofit Media kuwa mkewe alifanya uamuzi wa busara kumruhusu kumuoa binti huyo aliyempa ujauzito.

Mzee huyo alieleza kuwa hivi sasa anaishi na wake zake wote wawili kwa amani na kwamba wote wana furaha isiyo kifani.

Alisema hivi sasa anajenga nyumba kubwa zaidi itakayomuwezesha kuwafikia kwa pamoja wake zake huku akisifia utamaduni wa ndoa za mitala.

“Ni mimi pekee ninaeruhusiwa kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja kati yetu na kila mmoja wetu amekubaliana na hilo na analithamini, “alisema Mchungaji Thom ambaye anawaita wake zake kuwa ni dada- wenza.

 

 

Wakenya waandamana kupinga ufisadi, wapigwa mabomu
Messi amfunika Ronaldo Tuzo za La Liga