Mahakama ya Milimani nchini Kenya, imemuhukumu Mchungaji James Njuguna miaka 70 jela, baada ya kumpata na hatia ya kuwarubuni kwa kutumia maandiko ya Dini vibaya, na kufanikiwa kuwanajisi watoto wawili.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkuu wa Mahakama hiyo, Caroline Njagi baada ya vielelezo vya upande wa mashitaka kudhihirisha kuwa aliwanajisi watoto hao ndugu, wenye umri wa miaka 14 na 11 katika eneo eneo la Bondeni, Kajiado Kaskazini mwaka 2014.

Amesema, “Upande wa mashtaka ulithibitisha kesi hii kwa kiwango kinachohitajika dhidi ya mshtakiwa katika shitaka la unajisi katika shitaka la 1 na 2. hivyo Mshtakiwa anatiwa hatiani kama alivyoshitakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 215 cha CPC.”

Awali ilidaiwa kuwa, Njuguna alikuwa akiwaambia watoto hao kwamba sehemu zake za siri zina mafuta kutoka kwa Mungu na maji yaliyowaingia ni damu ya Yesu inawatakasa na watoto hao wawili walikuwa mashahidi wa waliothibitisha mbali na vipimo vya matibabu.

Usajili wa Hussein Abel nyuma ya pazia
Ligi Kuu Zanzibar rasmi Septemba 09