Imani ni kitu kikubwa sana ambacho kwa namna moja au nyingine hutusaidia kutupa muongozo wa maisha tunayoishi kwani wanasema hakuna ajuaye kesho yake, ila kwa imani zetu tayari tumejipangia majukumu tutayokabiliana nayo kesho, kesho kutwa, mwezi ujao hadi mwaka.

Dini nayo inachukua sura nyingine katika suala la imani kwani kumetokea manabii wa aina tofauti tofauti wanaokuja na mbinu mbalimbali wakidai kutukwamua kiimani na juu ya kuona ufalme wa Mungu, wapo wanaoamini na kufuata lakini pia wapo ambao hupingana juu ya imani hizo.

Mwaka jana mnamo Juni 8, 2018 mchungaji mmoja aliyefahamika kwa jina la Tito Watts na mkewe Amanda Watts, walikamatwa na polisi nchini kwao, Zimbabwe mara baada ya kuhujumu pesa za watu kwa kuwauzia tiketi walizodai kuwa ni tiketi za kuingia mbinguni.

Ambapo tiketi hizo zenye machapisho ya ”Ticket to Heaven” yaani tiketi ya mbinguni zilikuwa zinauzwa kwa gharama ya dola 500 ambayo ni sawa na milioni 1 na zaidi kwa pesa ya kitanzania.

Mchungaji huyo alitiwa mbaroni huku waumini wake wakiandamana na kutaka waachiwe wakidai kuwa ni wafuasi wa Mungu, na tayari idadi kubwa ya watu tayari imekwisha nunua tiketi hizo ambazo mchungaji alidai kuwa kila mwenye tiketi hiyo tayari amajiwekea nafasi mbinguni.

Hata hivyo mchungaji Tito wakati akihojiwa na polisi alisema hajali lolote linalosemwa na polisi hao na watu anachojiua ni kuwa anafanya kile ambacho Yesu Kristu amemtuma afanye hapa duniani.

”Yesu Kristu alinitokea na kunipa hizi tiketi zilizotengenezwa kwa dhahabu na kunitaka kuwauzia watu wote wanaotaka wokovu”.

Tickets-to-heaven

 

Video: Ndugai mtaka Zitto aache uongo, 'Haipendezi mtu mzima kuwa muongo'
Zitto: Mungu anipe nafasi ya kuongoza nchi yetu, amjibu Ndugai