Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashilika watu wawili akiwemo  mchungaji wa kanisa la
Pentekoste Gospel Mission la kibaha, Emanuel Paul Karata (35),
kwa ulaghai wa kutaka kupata waumini akisingizia mchawi amedondoka kwenye maombi ya mkesha wake na waumini.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, ACP Pius Lutumo amesema tukio hilo limetokea Agosti 24, 2023 na watu hao wanashikiliwa kwa mahojiano baada ya Basenga  Silvester Matheo (59), kudaiwa kudondoka kanisani akiwa anasafiri kwa ungo wa kishirikina na kuleta taharuki kwa waumini.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, ACP Pius Lutumo.

Amesema, “kulikuwa na ibaada ya mkesha ambapo mtuhumiwa akiwa na wenzake sita walidondoshwa kwa maombi na wenzake wakafanikiwa kutoroka kichawi, ili kuthibiti taharuki hiyo mchungaji alimchukua mtu huyo na vifaa vyake vya kishirikina na kumuweka ofisini kwake hadi asubuhi Polisi walipofika.”

Aidha, Kamanda Lutumo ameongeza kuwa Busenga alijinqsibu kuwa yeye na wenzake walifika kanisani hapo kishirikina kwa lengo la kupima imani ya waumini hao na katika mahojiano alidai kuahidiwa malipo ya shilingi 50,000 baada ya kutimiza lengo la ulaghai.

Kufuatia tukio hilo, Polisi Mkoa wa Pwani imetoa onyo kwa watu wenye tamaa ya kupata kipato cha haraka kwa kufanya ulaghai wa maombi, huku ikiwataka waumini kuwa makini na watu wachache wanaotaka kuharibu imani za
kidini kwa tamaa ya fedha.

CCM yatoa agizo Wahudumu wa kike Zahanati
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 31, 2023