Taasisi ya kuzuia na kupambana Rushwa TAKUKURU, mkoani Manyara inamshikilia mchungaji kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, Usharika wa Ufana, Emanuel Petro Guse, kwa kuendesha mikopo umiza bila kuwa na leseni ya biashara ya ukopeshaji fedha

Awali, TAKUKURU ilipata malalamiko kutoka kwa mkazi wa eneo la Bashnet aliyekopa shilingi 200,000 na kurejesha shilingi 500,000 lakini bado akawa anadaiwa shilingi laki nne na elfu themanini 480,000 kutokana na mkopo ule ule

TAKUKURU ilimtaka Mchungaji huyo kufika katika ofisi hizo lakini alikaidi na kuilazimu TAKUKURU kutuma makachero kwenda kumkamata na kumuhoji mtuhumiwa huyo ambaye alipinga kufanya biashara hiyo.

Makachero hao walifanya upekuzi ndani ya nyumba ya mchungaji na kubaini mikataba 48, ya mikopo umiza kisha kumchukua mpaka ofisi za TAKUKURU.

Mtuhumiwa alikiri ni kweli anafanya biashara hiyo ya mikopo umiza na kusema ni kweli alirudisha 400,000 na kudaiwa bado 480,000.

Mkuu wa TAKUKURU Manyara Holle Makungu amewaasa wakazi wa mkoa huo kutokubali kulipa riba kubwa na kukopa kwa watu wasio na leseni za serikali na kuwataka wale wote walioathirika na mikopo umiza ya mchungaji huyo wafike ofisi za TAKUKURU mkoa wa Manyara.

Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na TAKUKURU Mkoani manyara kwa uchunguizi zaidi wa mikataba hiyo.

JKCI yafanya upasuaji wa mshipa kwa mara ya kwanza
Keita aachiwa huru, Mali kuunda serikali ya mpito