Baada ya dirisha dogo la usajili Tanzania Bara kufungwa Januari 15,  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa orodha ya wachezaji wote waliosajiliwa na klabu mbalimbali hapa nchini.

Katika usajili huo kumekuwa na sapraizi kwa klabu ya Simba SC ambao katika wachezaji wao wawili waliosajiliwa kwa ajili ya Ligi Kuu na michuano mingine limekuwepo jina la nahodha wa DC Motema Pembe, Doxa Gikanji.

Usajili huo umezua gumzo kutokana na kutokuwepo tetesi za awali za ujio wake kama ilivyo kwa nyota wengine wa klabu kubwa za Azam, Young Africans na Simba SC.

Gikanji mwenye miaka 30 anayemudu nafasi ya kiungo mkabaji kwa sasa yupo na timu ya DR Congo nchini Cameroon kwenye michuano ya Mataifa ya Bingwa Barani Afrika ‘CHANA’ na atajiunga na Simba SC, baada ya michuano hiyo.

Simba SC imesajili wachezaji wawili katika dirisha dogo na kuleta maswali kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao wanahoji kwa nini jina la kiungo Mganda,  Taddeo Lwanga halipo na wakati  tayari walishatangaza kumsajili na walimtambulisha Desemba 02 mwaka jana.

Mwanafunzi auwawa kisa kuni
RC Gaguti atumia siku 5 tu kutekeleza agizo la Rais

Comments

comments