Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee amesema kuwa kinachopelekea wabunge wa chama chake kuhamia CCM ni tamaa zinazowaingia pindi wanapopewa dhamana na wananchi ya kuwatumikia na kudhani kwamba ubunge ni chanzo cha utajiri.

Amesema kuwa wabunge wote waliohama ni wale waliokimbilia kuchukua mikopo mikubwa bungeni na kupelekea kukatwa mishahara yote, kwahiyo kufanya vile ni kwaajili ya kunusuru hali zao kiuchumi.

Aidha, ameongeza kuwa wabunge wamekuwa wakijiingiza kwenye biashara bila kuwa na ufahamu juu ya vitu husika wanavyokimbilia kufanya, hivyo wengine huishiwa pesa na kushindwa kuhudhuria vikao vya bunge jijini Dodoma.

“Wanakosa uelewa juu ya dhamana waliyopewa na wananchi, matokeo yake wanaishia kukopa mikopo mikubwa hadi wanakosa hela za nauli wengine, mfano Waitara na huyo Ryoba wamepiga watu vizinga hadi wameamua kufika bei, CCM sio wao ni ugumu wa maisha”, amesema Mdee.

Hata hivyo, usiku wa Septemba 27, aliyekuwa Mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Chacha alitangaza kujiuzulu uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini na kusema kuwa amechukua uamuzi huo kumuunga mkono mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Dkt. Mpango apokea ripoti ya ukaguzi wa ununuzi wa Umma
JPM afanya uteuzi mwingine NIDA