Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee imeitaka Serikali kulipa deni linalodaiwa katika mifuko ya hifadhi za jamii ili iweze kuwa endelevu na wastaafu waweze kulipwa kwa wakati.

Mdee ameeleza hayo leo Aprili 16,  2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Amebainisha kuwa duniani kote mifuko hiyo huisaidia Serikali kufanya shughuli za maendeleo kwa kukopa kwa riba na  kulipa na kudai kuwa hapa nchini kuna changamoto kubwa ambapo Serikali na taasisi zake zinakopa kwa riba lakini hailipi.

“Usugu upo kwenye fedha zilizokopa. Kwanini mnakuwa na kigugumizi cha kulipa. Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) inaonyesha kuwa deni la Serkali ni Sh2.7 trilioni lakini haijajumuisha Sh1.7 trilioni za PSSF,” Amesema Mdee.

“ lakini kuna ugonjwa gani wa kulipa Sh1 trilioni kila mwaka za deni hilo ili mifuko iwe endelevu. Kwa mujibu wa vitabu vya CAG, Serikali imeingia makubaliano na sekta,  mifuko ya hifadhi ya jamii  ya kukopa fedha ambazo zimefika Sh10 trilioni.” amesema Mdee

Akitoa taarifa kwa Mdee Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Ajira, Kazi, Vijana na wenye ulemavu,  Jenista Mhagama  amesema Serikali inafanya tathmini ya mifuko ya jamii itakayoonyesha hali ya mifuko ili kupata hali halisi na nini kifanyike kwenye madeni inayodai.

Marekani na uwekezaji wa kishindo Tanzania
Watu 30 kushiriki mazishi ya mwanamfalme

Comments

comments