Mechi tatu zilizobakia zinatosha kuipa ubingwa timu ya Yanga endapo itashinda mechi hizo itakuwa imefikisha pointi 71 pointi ambazo hazitafikiwa na Simba hata kama watashinda mechi zao mbili zilizobaki ambazo zitawafanya wafikishe pointi 68.
Wakati ligi kuu Tanzania bara ikielekea ukingoni, mabingwa hao watetezi ndio timu pekee ambayo ipo kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu ukilinganisha na wapinzani wao Simba.
Yanga inaongoza ligi kwa wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa lakini wakiwa sawa kwa pointi na Simba wote wakiwa na pointi 62.
Mechi tatu za Yanga zilizosalia ndio zimeshikilia ubingwa wa 2016-17, ambao kama watautwaa itakuwa ni mara yao ya tatu mfululizo tangu walipochukua msimu wa 2014/2015, 2015/2016 na msimu huu 2016/2017 kama watafanikiwa kuuchukua.