Mchezo namba 20 wa ligi kuu Tanzania Bara kati Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar umerudishwa nyuma ambapo ulibidi upigwe September 17 sasa utachezeka September 13 kutokana na timu ya Taifa ya Tanzania kuingia kambini September 15 kujiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu kushiriki michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani CHAN.

Mchezo  wa kwanza wa Tanzania dhidi ya Sudan utachezwa Septemba 20 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku mchezo namba 18 kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Azam Fc umeondolewa kwenye ratiba ili kuipa nafasi klabu ya Azam kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho.

Lakini pia mchezo namba 19 kati ya Coastal Unioni dhidi ya KMC nao umerudishwa nyuma kutoka September 18 hadi September 13 huku michezo ya Raundi ya tatu ya ligi kuu Tanzania Bara kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga, Simba baina ya Lipuli, Polisi Tanzania dhidi ya KMC, Coastal Union dhidi ya Azam nayo imeahirishwa kutokana na mchezo wa kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani mchezo ambao utachezwa September 20.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 10, 2019
Alichosema Ndugai juu ya uamuzi wa mahakama kesi ya Lissu