Baada ya The Game, Meek Mill amekuwa mtu wa pili ambaye amempa ushauri Tekashi 69 kuhusu matatizo yake ya kisheria ambayo amekuwa akiendelea nayo, kitu kinachomfanya kupitia wakati mgumu kipindi hiki anachopitia umaarufu na kwamba anatakiwa kufata sheria zinavyotaka

Kwenye mahaojianao na kituo cha radio Real 92.3 Meek Mill amesema kuwa Tekashe 69 ni kijana mzuri sana lakini anapaswa kupunguza makundi ya kihuni kwa kipindi hiki anachopitia,

“Hakuna mtu anaetaka kuishi kama vile huwezi kuishi na walinzi 10 maisha yote watu wanafahamu kuwa hahusiki na vitu vyote ambavyo marafiki zake wanafanya, lakini yeye ndio anaonekana kama kiongozi kulingana na umaarufu na yeye ni kioo cha jamii,”amesema Meek Mill

Ameongeza kuwa angeweza kumwambia mambo anayofanya Tekashi 69 ni changamoto za muziki hivyo anapaswa kupunguza kasi kwa sababu anakosana na watu wengi sana kwa sasa kulingana na makundi aliyokuwa nayo pia muziki wa hip hop unahitaji upinzani ila anatakiwa kuwa makini sana.

Serikali kulipa bilioni 4 kila siku kwa wakulima wa Korosho
Msongamano wa wafungwa Magerezani wamchefua Jenerali Kingu

Comments

comments