Wafuasi wa upinzani nchini Armenia jana wameandamana katika mji mkuu wa Yerevan, wakimtaka waziri mkuu ajiuzulu, kutokana na jinsi alivyoshughulikia mzozo wa Nagorno-Karabakh na nchi jirani ya Azerbaijan.

Wanasiasa wa upinzani na wafuasi wao wanamtaka Nikol Pashinyan ajiuzulu kufuatia makubaliano ya amani ya Novemba 10 ambayo yaliipa Azerbaijan udhibiti wa sehemu kubwa ya jimbo la Nagorno-Karabakh na maeneo ya karibu. 

Makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Urusi yalimaliza siku 44 za mapigano makali, ambayo jeshi la Azerbaijan ilivishinda vikosi vya Armenia. 

Maelfu wa waandamanaji walishiriki katika maandamano na wengine kuvamia majengo ya serikali amabpo viongozi wa maandamano hayo wanasema waandamanji watapiga kambi kwenye uwanja mkuu wa Yerevan hadi waziri mkuu Pashinyan atakapoondoka madarakani.

Mbunge wa Arusha ahoji maduka 15 kufungwa kwa kudaiwa kodi
Dkt. Ndungulile ayageukia makampuni ya simu