Meli ya mizigo iliyokuwa imebeba magari ya kifahari takribani 4,000, imezama katika Visiwa vya Azore
nchini Ureno, zikiwa zimepita wiki mbili tangu iliposhika moto.

Meli hiyo iitwayo Felicity Ace, ilikuwa ikisafirisha magari hayo ya kifahari, yakiwemo aina ya Porsches na
Bentleys na ilikuwa njiani kuelekea Kisiwa cha Rhode nchini Marekani kutokea bandari ya Ujerumani ya
Emden wakati moto ulipozuka.

Nahodha katika moja ya bandari iliyo karibu katika Kisiwa cha Faial, Joao Mendes Cabecas, amesema wahudumu wote wa meli hiyo waliokolewa wakati moto huo ulipoanza Februari 16, lakini Maelfu ya magari ya kifahari yameachwa kwenye meli hiyo baada ya kushika moto katika Bahari ya Atlantiki ikielekea Marekani.

Ameliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba hakuna uvujaji wa mafuta ulioripotiwa hadi sasa lakini amesema kuna hofu kwamba matenki ya mafuta yanaweza kuharibika wakati chombo hicho kikiwa chini ya Bahari ya Atlantic, katika
kina cha mita 3,500.

Jeshi la wanamaji la Ureno limesema hakuna aliyejeruhiwa na moto huo na kwamba wafanyakazi wote 22
wa meli hiyo walipelekwa katika hoteli moja baada ya jeshi la wanamaji, meli nne za wafanyabiashara
waliokuwa wakisafiri katika eneo hilo na Jeshi la Anga la Ureno kukamilisha zoezi hilo la kuwaokoa.

Meli hiyo iliyopewa jina la Felicity Ace, ilikuwa ikisafiri kutoka Emden nchini Ujerumani kabla ya kushika moto kwenye ufuo wa visiwa vya Azores nchini Ureno.

Gazeti la Ujerumani la Handelsblatt liliripoti kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba magari 3,965, ambayo pia ni pamoja na Audi, Lamborghini na idadi ndogo ya Bentley.

“Mmiliki wa meli Felicity Ace anawasiliana na wakala husika ili kuandaa mpango wa kuivuta meli, Hadi sasa, hakuna chanzo cha uchafuzi wa mazingira kilichorekodiwa.” jeshi la wanamaji lilisema katika taarifa.

Meli hiyo iliyopewa jina la Felicity Ace, ilikuwa ikisafiri kutoka Emden nchini Ujerumani kabla ya kushika moto kwenye ufuo wa visiwa vya Azores nchini Ureno.

Marekani yatoa mapipa milioni 30 ya mafuta kunusuru ulimwengu
Njia za kielektroniki za malipo kufungwa