Meli kubwa iliyonama baharini na kusukumwa na mawimbi makubwa imeendelea kuzua taharuki nchini Ufaransa huku juhudi za kuibembeleza iweze kufika pwani ya Ufaransa zikiendelea baada ya juhudi za kuisimamisha kuzidi kushindikana.

Meli hiyo inayojulikana kama  MV Modern Express, imebeba mzigo mkubwa wa takribani tani 3,600 zikiwamo mbao, mafuta na mashine nyingine za uchimbaji ilianza kuinama tangu Jumanne ya wiki iliyopita baada ya kupata hitilafu katikati ya bahari ya Atlanta.

Tayari marubani 22 wa Meli hiyo wameondolewa. Maafisa wa Ufaransa wanaeleza kuwa leo wanaweza kufanya jaribio la mwisho kabisa la kuisimamisha ingawa matumaini yanaendelea kupotea.

Endapo itashindwa kusimama, meli hiyo iliyoinama kati ya nyuzi 40 na 50 inatarajia kugonga ufukwe wa Ufaransa kati ya leo usiku na kesho kama itaendelea kuwa salama.

chanzo: BBC

 

 

Picha: Madaktari wafanikiwa kuwatenganisha mapacha waliozaliwa wameungana
Serikali yapiga 'stop' shule binafsi kupandisha Ada