Kocha Mkuu wa Dodoma liji, Melis Medo amewaomba wachezaji wake kutobweteka kwa nafasi waliyopo kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, badala yake waongeze juhudi kukusanya pointi zaidi.

Dodoma Jiji inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 15 katika michezo 11 iliyocheza hadi sasa.

“Nadhani wachezaji wameridhika na nafasi ya sita tuliyopo, ukweli siridhiki na mwenendo wao na wanapaswa kubadilika sababu ligi bado ni ndefu tunapaswa kukusanya pointi za kutosha ili zije kutusaidia huko mbeleni wakati ushindani utakapoongezeka,” amesema Medo.

Amesema malengo yake ni kuiona Dodoma Jiji inamaliza msimu huu kwenye nafasi za juu ikibidi kupata uwakilishi kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao.

Medo amesema yeye na msaidizi wake Kassim Liogope watajitahidi kupambana kurekebisha mapungufu yaliyopo ili kubadili mwenendo wa timu hiyo na kupata ushindi kama ilivyokuwa kabla ya ligi kusimama katika kalenda ya FIFA.

Huu ni msimu wa nne kwa Dodoma Jiji kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, na katika kipindi chote hicho timu hiyo imekuwa ikimaliza nafasi za katikati mwa msimamo wa ligi hiyo ingawa msimu huu ineonesha nia ya kutoa ushindani kwa timu zinazowania ubingwa Simba, Young Africans na Azam FC.

Bacca aahidi mambo mazito Young Africans
Mikel Arteta alipongeza jeshi lake