Waziri wa zamani wa Mamboya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amekaribishwa kujiunga na Chama Cga Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiwa ni siku chache tangu atoe maoni yake akiikosoa serikali ya Rais John Magufuli.

Mwanasiasa huyo mkongwe amekaribishwa na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob ambaye alimshawishi kwa kutumia mifano ya wanasiasa wakongwe waliokuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliohamia Chadema na Ukawa kwa ujumla akiwemo Edward Lowassa, Frederick Sumaye na Kingunge Ngombale Mwiru.

Watu hawashangai alichosema Membe kwa sababu sio hoja ngeni, zimesemwa sana na wapinzani. Wanachoshangaa ni yeye kusema hayo. Hafanani na hoja anazoziongea,” Jacob aliliambia gazeti la Mwananchi katika mahojiano maalum.

“Asiwe vuguvugu, hicho ndicho kinachompa shida. Kama anataka kuja huku asiwe na wasiwasi, chama changu kitampokea na hata hayo anayoongea yatakuwa na mantiki na watu watamsikiliza kwa sababu ni mpinzani,” aliongeza Meya huyo wa Kinondoni.

Hivi karibuni, Membe aliingia katika mgogoro wa maneno na baadhi ya makada wa CCM kutokana na namna alivyokosoa utendaji wa serikali ya awamu ya tano hususan katika suala la kubana matumizi katika uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Safari za nje ya nchi na namna ya inavyofanya kazi na wafanyabiashara.

 

Idris aweka wazi mwezi ambao yeye na Wema wanatarajia kupata mtoto
Lukuvi Atumbua Ghorofa refu jijini Dar es Salaam