Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe amesema kuwa anashangazwa na matukio ya utekaji yanayoendelea kutokea hapa nchini, huku akiwataka viongozi wa vyama, serikali na dini kukemea matukio hayo.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa wimbi la utekaji linaloendelea hapa nchini linapaswa kukemewa hadharani na viongozi wa ngazi zote,

”Mimi naona huu ni utamaduni mpya ambao haukubariki, na ningependa kuchukua nafasi hii kusema tu kwamba,  suala la utekaji ama watu kupotea linaweza kuiharibia nchi yetu heshima duniani,” amesema Membe.

Aidha, ameongeza kuwa hatuwezi kuendelea kuishi kwenye nchi ya watu wenye wasiwasi na uoga na wasiojua kesho wataamka vipi na ajenda hiyo ya utekaji ametaka iishe maana isipoisha itaenda mpaka kwenye uchaguzi.

Hata hivyo, Membe amewaomba viongozi wa chama na serikali kulifikiria suala hilo na kulikemea ili lisitokee, na wajifikirie wao wenyewe kama watoto wao wangekuwa wanatekwa wasingeweza kupata hata watalii kutoka nchi mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Membe ameonyesha kutokubaliana na uamuzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai wa kumvua nafasi ya ubunge, mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu juni 28 mwaka huu.

Ninauhakika kwamba Lissu atakaporudi ataenda mahakamani na kama kuna haki ataipata tu huko.

 

Simba yazidi kujiimarisha, yashusha kifaa kutoka TP Mazembe
Julai 7 ya msanii Diamond Platnum ipo hivi