Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM kilichokitana leo Machi 31 mkoani Dodoma kimemsamehe alieyewahi kuwa waziri wa Mambo ya nje Benard Membe na kumrejeshea uanachama.
Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM itikadi na uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema, msamaha huo ni kwa mujibu wa Ibara ya 48 kifungu cha 8 cha katiba ya CCM.
Aidha wamezingatia maombi ya barua zake za kuomba msamaha kwa chama Alipoulizwa kama ameomba kurudishiwa uanachama, Shaka amesema, Membe amewahi kuandika barua mara tatu kuomba kurejeshewa uanachama wake na sasa NEC imeamua kumrejeshea hadhi hiyo aliyoondolewa tangu mwaka 2018.
Sambamba na hayo NEC pia imemrejeshea uanachama Abdallah Maulid diwani ambaye amewahi kuwa muwakilishi wa jimbo la Jang’ombe ambaye nae aliondolewa hadhi hiyo sambamba na Membe mwaka 2018