Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe amezungumzia kile kilichopewa jina la ‘kilio’ cha aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.

Kilio hicho ni kauli ya Lowassa aliyoitoa siku kadhaa zilizopita alipokuwa wilayani Monduli akidai kuwa serikali imekuwa ikiwaandama wafanyabiashara waliokuwa wakiunga mkono harakazi za vyama vya upinzani wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.

“Sio dhambi wafanyabiashara kufadhili vyama vya siasa wakati wa uchaguzi. Lakini akishapatikana Rais, Serikali inawakusanya wafanyabiashara wote na kufanya nao kazi ya ujenzi wa Taifa na sio kuwaburuza,” alisema Membe katika mahojiano maalum na gazeti la Mwananchi.

Mrembo wa UDSM aliyedaiwa kuwa Msukule uliokutwa shimoni anena kwa uchungu
Diamond adai mtoto wake anawazidi pesa wasanii hawa wa Bongo