Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT – Wazalendo Bernard Membe amesema afya yake imeimarika na yupo tayari kwa ajili ya kuanza kampeni za Urais. 

Membe amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo amewatarifu wanachama na watanzania wote kuwa anatarajia kuwasili leo Septemba 15 nchini akitokea Dubai.

“Afya yangu imeimarika na sasa nipo tayari kwa kampeni za Urais,  inayoanzia Tabora wiki hii hadi Oktoba 26”ameandika Membe.

Aidha ameongeza kwa kuwataarifu watanzania na wanachama wa ACT – Wazalendo kuwa atawasili Dar Es Salaam saa 8:40 mchana akitokea Dubai.

Awali Bernard Membe alizindua kampeni zake katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.

UCHAGUZI 2020: NEC yakemea wanasiasa
PSG wapambania haki, kushirikiana na LFP

Comments

comments