Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na kada wa CCM, Bernard Membe, rasmi amejiunga na chama cha upinzani ACT- Wazalendo.
Uanachama wake mpya umetangazwa leo na kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe katika mkutano wa wanahabari na wadau wengine uliofanyika katika mtandao wa Zoom.
Membe amesema amejiunga kama mwanachama wa kawaida lakini yuko tayari kutumikia chama hicho kwa ngazi na namna yoyote ile.
“Kilichonivutia katika chama cha ACT-Wazalendo ni katiba ya chama hicho na itikadi yake ya kutaka kuleta mabadiliko,” amesema Membe
Aidha Zitto Kabwe amemtia moyo Membe kuchukua fomu kuwania nafasi ya uongozi.
Membe aliitikia kwa kuahidi kwamba atakuwa tayari kushiriki katika kinyang’anyiro cha uchaguzi.
“Watanzania watafurahia uchaguzi huu ujao,” ameahidi Membe.