Meneja wa Kikosi cha AC Milan ya Italia Stephen Pioli, amefunguka juu ya Mshambuliaji kutoka nchini Ureno Rafael Alexandre da Conceição Leão kwamba atakuja kuwa mchezaji wa daraja juu duniani.

Leao amekuwa ni miongoni mwa Wachezaji Bora wa AC Milan ambapo msimu uliopita aliisaidia kuipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia ‘Seriea A’.

Kocha Pioli amesema: “Rafa atakuja kuwa mchezaji wa daraja la juu kabisa duniani kama akiendelea na kasi yake.”

Hata hivyo, Milan kwa sasa inapambana kuona ni namna gani inakamilisha dili la mkataba mpya wa nyota huyo.

Mkataba wa sasa wa Leao unatarajiwa kumalizika 2024 na Milan inataka kuona anasalia hapo.

Hivi karibuni, Leao alinukuliwa akisema: “Nataka kusalia Milan. Lakini pia kwa msimu huu nimekuwa shabiki mkubwa wa kiungo Mshambuliaji wa SSC Napoli Khvicha Kvaratskhelia, kwa sababu napenda ujuzi wake na hana tofauti kubwa na mimi hasa tunapokuwa uwanjani.”

AC Milan ilimsajili Leao mwaka 2019 akitokea nchini Ufaransa alipokuwa akiitumikia klabu ya Lille, ambayo aliitumikia katika michezo 24 na kufunga mabao manane.

Kabla ya hapo Leao alikuwa akiitumikia klabu ya nyumbani kwao Ureno Sporting CP ambayo iliamua kumpandisha kutoka kikosi cha vijana cha klabu hiyo mwaka 2017, ambapo alicheza michezo mitatu na kufunga mabao matatu.

Akiwa katika kikosi cha vijana cha klabu hiyo Leao alicheza michezo 12 na ufunga mabao 07.

William Saliba bado majanga Arsenal
Ansu Fati hatarini kuondoka FC Barcelona