Meneja wa Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo Tuisila Kisinda, amekata mzizi wa fitna ndani ya klabu ya Young Africans kuhusu uhalali wa mchezaji huyo.

Nestor Mutuale ambaye ni meneja wa Kisinda anayewindwa na klabu ya RS Berkane ya Morocco, amesema mchezaji wake ni mali halali ya Young Africans na sio kama invyoripotiwa na baadhi ya wadau wa soka la Bongo.

Mutuale ametoa ufafanuzi huo, kufuatia tetesi zilizoibuka juzi Jumatatu na jana Jumanne, ambapo baadhi ya wadau wa soka la Bongo walidai ofa ya Kisinda kutoka RS Berkane imetumwa kwenye klabu yake ya DR Congo AS Maniema na sio Young Africans.

Madai hayo yalikwenda mbali zaidi kwa kuelezwa kwamba, Kisinda yupo Young Africans kwa mkopo akitokea AS Maniema ambayo pia iliwahi kumtoa kwa mkopo kwenda AS Vita Club.

Mutuale amesema endapo Kisinda atauzwa kwenye klabu ya RS Berkane, asilimia kubwa ya fedha itachukuliwa na Young Africans na nyingine kiasi itakwenda AS Maniema, kutokana na mkataba uliopo kisheria.

“AS Manyema itanufaika kwa kuwa Kisinda alikuwa ni mchezaji wao na ni sehemu ya makubaliano.”

“Watu waelewe Kisinda alikuwa akicheza AS Vita kwa mkopo akitokea AS Maniema, hivyo Yanga walimsajili kutoka Maniema.”

“Hata Tonombe Mukoko ni mchezaji wa Yanga walimsajili kutoka AS Vita, ofa zinazotumwa zote zinaenda Yanga, hata Sasa hivi ipo ofa kutoka Tunisia, Yanga wakikubali wao ndio watapokea pesa, hayo maneno mengine ni uzushi mtupu Mimi ndiye meneja wa wachezaji wote hao” amesema Nestori Mutuale.

Bahasha yenye risasi 3 yatumwa kwa papa francis Vatican
Al Ahly kama Simba SC 'HAWAKWEPESHI'