Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi, amekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni zikiwa na kichwa cha habari kinachosomeka “Mengi ajitoa kwa Lowassa.”

Dk. Mengi ameikanusha taarifa hizo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Alisema taarifa hizo zilizokuwa zinaeleza kuwa yeye amesema mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa hawezi kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ni za upotoshaji.

Taarifa hizo zilionekana kubeba kauli ya Dk. Mengi zikidai amesema kuwa wapinzani hawawezi kushinda uchaguzi mkuu labda baada ya miaka kumi.

“Nasikitika kusema kwamba taarifa hiyo ni ya uongo, upotoshaji na ya uchochezi. Taarifa za namna hii zisipokemewa na kuchukuliwa hatua za haraka, zitaathiri amani ya taifa letu. Ni matarajio yangu kwamba vyombo husika vitachukua hatua zinazostahiki kwa haraka iwezekanavyo. Nawashukuru sana, asanteni,” alisema.

Picha: Lowassa Alivyoitikisa Musoma, Mapokezi Yavunja Rekodi Kwa 'Mbwembwe'
Sumaye Aweka Tena Richmond Mezani