Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amemkosoa vikali Rais wa Marekani Donald Trump kwa hatua yake ya kukataa kuidhinisha azimio la mkutano wa kilele wa kundi la G7.
Merkel amesema kuwa Ulaya haitaendelea kudhulumiwa kuhusiana na masuala ya kodi ambayo yamezua utata katika mkutano huo.
Aidha, Trump ambaye alikuwa kiongozi wa mwisho kuwasili katika mkutano huo na wa kwanza kuondoka, alitangaza kupitia mtandao wa twitter kwamba amewaamuru maafisa wake kubatilisha uamuzi wa awali wa kuunga mkono tangazo la mwisho la mkutano huo.
”Umoja wa Ulaya utasonga mbele kutangaza hatua za kulipa kisasi dhidi ya uamuzi wa Rais Trump kuziwekea adhabu ya nyongeza ya ushuru kwa bidhaa za chuma na bati, kwa sababu hatuwezi kuruhusu kuendelea kudhulumiwa,”amesema Merkel.
Hata hivyo, Umoja wa Ulaya na Canada ambayo pia imewekewa ongezeko la ushuru, zinatarajia kutangaza hatua za kulipiza kisasi dhidi ya Marekani ifikapo Julai 1 mwaka huu.
-
Trump akomaa na msimamo wake dhidi ya nchi za Ulaya
-
Wavuvi haramu kutoka Tanzania wakamatwa nchini Kenya
-
Rais Putin kuteta na Rais wa China