Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amemkaribisha Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron kwenye mazungumzo yanayolenga kuimarisha mageuzi yanayoweza kuzuia kusambaratika kwa Umoja wa Ulaya, huku mzozo wa uhamiaji ukiendelea.

Viongozi hao wawili wa mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya wanasaka muafaka kati ya mtazamo wa Macron kuelekea mageuzi makubwa ndani ya Umoja wa Ulaya na ule wa Ujerumani ambayo inataka pachukuliwe tahadhari kubwa.

Aidha, Merkel na Macron, kwa pamoja, wamesisitiza kuwa Rais Donald Trump wa Marekani anaonekana waziwazi kuutishia Umoja wa Ulaya kwa vita vya kibiashara na sera za ulinzi na mabadiliko ya tabia nchi.

Hata hivyo, viongozi hao wakiwa wasemaji na watetezi wakubwa wa muungano wa Ulaya, Merkel na Macron wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wanasiasa wa siasa kali kwenye mataifa yao na kwenye serikali za Italia, Austria, na nyingine kadhaa za Ulaya Mashariki.

 

 

Canada yaidhinisha matumizi ya Bangi hadharani
Alichoongea Diamond kuhusu media zisizofanya kazi zake