Mtu mmoja, Meshack Azikam (23), mkazi wa kichangani Manispaa ya Morogoro anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za wizi wa misalaba 14 ya makaburini.

Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, ACP. Alex Mkama amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa aking’oa msalaba katika makaburi ya Kola yaliyopo Manispaa ya Morogoro na baada ya kumfanyia upekuzi nyumbani kwake walikuta misalaba mingine 13.

Msimamizi wa makaburi hayo, Abdalah Salum amesema changamoto hiyo imekua kubwa katika eneo hilo na mara nyingi wizi unafanyika majira ya alfajiri na jioni, ambapo licha ya kuiba misalaba pia limeibuka wimbi wa wizi wa matofali na marumaru.

Amesema, “tumeshawakamata wezi mara nne kwa nyakati tofauti na wengine tumewapeleka polisi wengine tumewafikisha mahakamani na misalaba mingine ipo hapa tumekutwa imeng’olewa na kutelekezwa katika makaburi hayo tunaomba ndugu waje wachukue wakurudishie kwenye makaburi a ndugu zao.”

Tishio la Simba: Wananchi watakiwa kutotembea usiku
Kakolanya: Wabongo tujifunze kwa Chama, Diarra